Thursday , 20th Jul , 2023

Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji Derick Mosha amesema TPDC inatarajia kupeleka gesi katika nchi za Kenya, Uganda na Zambia na pia kujenga maghala makubwa ya kuhifadhia mafuta ili Tanzania iwe kituo kikuu cha mafuta kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini

Maghala ya mafuta

Hayo yamesemwa wakati wa mkutano na wahariri wa vyombo vya habari ulioandaliwa kwa ushirikiano na Ofisi ya Msajili wa Hazina

Aidha serikali kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) linakusudia kuhakikisha usafiri wote umma zikiwemo daladala, bajaji, bodaboda pamoja na mabasi na malori yanatumia gesi asilia badala ya mafuta ili kupunguza uchafuzi wa mazingira

Ili kufanikisha hilo  TPDC inatarajia kujenga vituo vya kutosha vya kujaza gesi ambapo kituo kikuu kitajengwa eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam ujenzi ambao utachukua miezi nane kukamilika.