Friday , 14th Jul , 2023

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewataka Watanzania hususani vijana kuacha kufanya ngono zembe ili kuondoa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na UKIMWI wenyewe.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete

Akizungumza kwenye ya kuwaaga wapanda mlima na waendesha baiskeli kwenye kampeni ya kuchangisha fedha dhidi ya VVU/UKIMWI iliyofanyika Machame, mkoani Kilimanjaro Kikwete amesema umefika wakati wa kueleza ukweli kwa jamii kuhusu hali halisi ya maambukizi ya ugonjwa huo

"Nilipokuwa Rais nilikuwa naendesha sana kampeni, kukumbusha Watanzania jamani eeeh! UKIMWI upo! ni maradhi ya kujitakia si maradhi ya bahati mbaya tusimsingizie Mwenyezi Mungu, hapana, ile njia kuu inayosambaza UKIMWI tunapanga mahali pa kukutana, tunapanga siku ya kukutana, tunapanga na saa ya kukutana labda aliyebakwa tu…usisahau kinga," amesema Kikwete.

 Aidha Kikwete amesema kwa sasa juhudi mbalimbali za serikali zinaendelea kama awamu nyingine zilivyofanya kupambana na maradhi ya Ukimwi kutoka asilimia nane hadi asilimia 4.7 iliyopo Sasa.