Friday , 14th Jul , 2023

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ni mgonjwa na yuko nchini Urusi kwa ajili ya matibabu

Taasisi ya Rais huyo imesema kuwa Zuma atarejea Afrika Kusini mara tu madaktari wake watakapomaliza matibabu

Taarifa hii imetolewan siku moja baada ya Zuma kushindwa kesi katika Mahakama ya Kikatiba kesi ambayo alikuwa akijaribu kubatilisha uamuzi kwamba ni lazima arejee gerezani.

Mahakama ya Kikatiba nchini humo imesema Zuma alipewa msamaha wa matibabu kinyume cha sheria
Zuma alikuwa amepewa msamaha na mkuu wa zamani wa huduma ya magereza, Arthur Fraser lakini sasa mahakama imebatilisha tena na anatakiwa kurejea Gerezani

Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance kimefurahishwa na uamuzi wa mahakama ukisema kwamba unathibitisha kuwa Zuma "anatakiwa kuwa gerezani".