Thursday , 13th Jul , 2023

Wananchi wa vijiji vya Ilolo na Nanguchile Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi, wamelalamika kupigwa, kuvunjiwa nyumba na mali zao lakini pia mazao yao kugeuzwa kuwa sehemu ya malisho na wafugaji jamii ya Wamang’ati ambao walivamia vijiji hivyo nyakati za usiku

Wakulima wanasema usiku wa saa mbili walishangazwa na shambulio la ghafla lililofanywa na wafugaji hao kwa kuteka maeneo na kuwashambulia vibaya wananchi, huku wengine wakivunja nyumba na kuibiwa fedha kwenye maeneo ya biashara kwa nguvu

Baadhi ya wakulima wamelazwa katika Hospitali ya Misheni ya Mnero Wilayani Nachingwea Wanasema, hawakufanya jambo lolote lililowatia hasira Wafugaji, sababu ya wao kushambuliwa na jamii hiyo ya Wamang’ati ni kuzalisha mazao ya Mbaazi ambayo wafugaji huamini hiyo ni lishe nzuri kwa Wanyama kwas ababu huwasaidia kutoa maziwa kwa wingi.