
Waziri wa Elimu Adolf Mkenda
Profesa Mkenda ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea kituo cha sayansi cha Stem park kilichopo jijini Tanga, mpango ambao amesema utasaidia kumaliza tatizo la wanafunzi kutopenda masomo ya sayansi.
Waziri Mkenda amesema kituo ambacho kitajengwa mjini Dodoma kitakuwa kama kituo cha mfano ambacho wabunge na viongozi wengine wa serikali watakitembelea ili kuona umuhimu wa kuwa na vituo vya aina hiyo kwenye maeneo yao.
"Dodoma ni katikati ya nchi yetu halafu pale wabunge, mawaziri wenzangu na watu mbalimbali wakuu wa mikoa nitapenda watembelee pale waone nini kinaweza kufanyika vituo hivi vinapaswa kujengwa kila mikoa najua haitafikia wanafunzi wote vitu vyote hivi ni matumda ambayo yanapatikana kkirahisi, "alisema Waziri Mkenda.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Project Insipire Lwidiko Edward amesema kituo hicho kinawatengeneza wanafunzi kwenye masomo ya sayansi kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo kujifunza kwa miradi na kuandaa mazingira yanayotoa hamasa ya kusoma.
Mpango wa ujenzi wa vituo hivyo unakuja wakati kukiwa na ari ndogo ya wanafunzi wanaopenda masomo ya sayansi ambao wengi wamekuwa wakikimbilia masomo ya sanaa kutokana na mazingira duni ya kujifunza masomo hayo.