Friday , 7th Jul , 2023

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 46 wamenusurika kifo baada ya kutokea ajali katika eneo la Balili kona wilayani Bunda mkoani iliyohusisha gari aina ya Tata la kampuni ya Johamvia linalofanya safari zake kutoka wilayani Serengeti kwenda mkoani Mwanza.

Gari iliyopata ajali

Wakizungumza na #EastAfricaTV baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wanasema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi ambapo gari lilipofika katika kona lilimshinda dereva na kuanguka mtaroni.

"Sisi tulikuwa tumekaa pembeni ya mwa barabara ambapo tuliliona gari hilo likija kwa mwendokasi lakini alipotaka kukata kona ikamshinda na kuanguka," amesema shuhuda

Kwa uapande wao baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wameelezea namna ambavyo ajali hiyo imetokea.

Akithibitisha kupokea majeruhi wa ajali hiyo Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Bunda Pendo Faustine, amesema wamepokea majeruhi 46 na maiti moja huku mkuu wa wilaya ya Bunda Vincent Naano akiwaonya madereva juu ya mwendokasi.