Waziri wa Nishati January Makamba
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nishati January Makamba, amesema kuwa bwawa hilo lenye Mita za ujazo bilioni 30 mpaka siku ya jana maji yaliyoingia ndani ya bwawa hilo yalikuwa na Mita za ujazo bilioni 13.8 sawa na asilimia 43 hivyo ni hatua nzuri ya utekelezaji wa ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) lililopo rufiji.
"Ndani ya msimu mmoja wiki iliyopita tulifikia kina cha chini cha kuzalisha umeme katika Bwawa wa Julius Nyerere, kina cha bwawa lote lile ni Mita 184 kutoka usawa wa bahari, kina kinachotakiwa ili bwawa lianze kuzalisha umeme ni mita 163. 61 kutoka usawa wa bahari maana yake ni kwamba tumefika na tumepita kina kinachotakiwa kuzalisha umeme," amesema Waziri Makamba
Aidha, Makamba amesema kuwa serikali imeanza mchakato wa kujadili usalama wa bomba la kusafirisha mafuta linalotoka Kigamboni Tanzania mpaka Ndola Zambia ambalo mwanzoni lilikuwa likisafirisha mafuta ghafi na hivi litasafirisha mafuta ya dizeli.