
Wenyeji walijaribu kumwokoa lakini hawakuweza licha ya kupata msaada kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya. Mwili wake ulipatikana baadaye na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Kinara.
Rafiki wa marehemu amewalaumu wenzake kwa kukimbia eneo la tukio baada ya kuona kuwa kuta zimeanguka akidai kwamba kama wangebaki au kupiga kelele kwa msaada labda wangemwokoa.