Thursday , 29th Jun , 2023

Kiongozi mwandamizi wa chama cha upinzani cha Congress Rahul Gandhi katika jimbo la Manipur lililokumbwa na ghasia nchini India amezuiliwa na polisi.

Gandhi yuko katika jimbo la kaskazini mashariki kwa ziara ya siku mbili kukutana na watu waliokumbwa na ghasia pamoja na kukutana na viongozi wa makundi ya kiraia.

Kwa miezi miwili iliyopita, Manipur imekuwa ikikabiliwa na mapigano kati ya jamii nyingi za Meitei na Kuki.Zaidi ya watu 100 wamefariki na wengine zaidi ya 400 wamejeruhiwa hadi sasa. Waziri Mkuu Narendra Modi amefanya mkutano na maafisa wa juu wa serikali ili kutathmini hali ya Manipur lakini amekosolewa kwa kutotembelea jimbo hilo au kutoa maoni juu ya hali hiyo.

Karibu mwezi mmoja baada ya ghasia kuanza, Waziri wa Mambo ya Ndani Amit Shah alitembelea jimbo hilo kuweka mpango wa kurejesha hali ya kawaida, lakini matukio mapya ya vurugu yanaendelea kuripotiwa karibu kila siku.

Baada ya kuwasili katika mji mkuu Imphal siku ya Alhamisi asubuhi, Gandhi alikuwa amechapisha ujumbe wa Facebook akisema kuwa "kurejesha amani ni kipaumbele cha juu. Manipur inahitaji uponyaji, na kwa pamoja tu tunaweza kuleta maelewano.", lakini baadae polisi waliingilia kati na kumzuia kuzuru eneo hilo