Monday , 26th Jun , 2023

Mtoto aitwaye Haruna Mwanakatwe anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kumi (10) mlemavu wa viungo na mkazi wa mtaa wa Edeni B Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa ameuawa kwa kuliwa na Nguruwe nyumbani kwao.

Nguruwe

Tukio hilo limetokea jana Juni 25, 2023, baada ya mtoto huyo kubaki ndani peke yake na kwamba alijisaidia na kukosa msaada hivyo inadaiwa Nguruwe aliposikia harufu ndipo alipoenda kuvamia  chumba alichokuwepo mtoto huyo na kuanza kumshambulia miguuni, tumboni na sehemu za siri.

Kwa upande wa wanafamilia ya mwanakatwe wanakanusha skendo ya kutokumjali marehemu huku diwani wa kata hiyo akitoa wito kwa wananchi kutokufuga mifugo ndanio ya nyumba zao.