Wednesday , 21st Jun , 2023

Watu wawili wamejeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa matibabu baada ya lori la mafuta walilokuwa wakichomelea kulipuka katika kituo cha mafuta cha Infinity eneo la Mafiati Jijini Mbeya

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya, Mrakibu  Gervas Fungamali amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa Kikosi cha Zimamoto kimefanikiwa kudhibiti moto ili usilete madhara zaidi

Mlipo huo umehusha gari namba T 298 CKF aina Howo yenye tela namba T407 BCN ambalo lilikuwa linachomelewa