Tuesday , 20th Jun , 2023

Familia ya Mohamed Ramadhan aliyekuwa mkazi wa Mtaa wa Magomeni Kagera, wameiomba serikali kuwasaidia kuupata mwili wa ndugu yao aliyefariki akipatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili, na ndugu kushindwa kulipa gharama za matibabu ya ndugu yao.

Tangu June 15, 2023 Marehemu Mohamed Ramadhan (49) alifariki wakati akipata matibabu baada ya kupata ajali ya kugongwa na bajaji huku familia wakikiri kushindwa kulipa gharama za matibabu wanazodaiwa, ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 5. 

Marehemu hajaacha mke wala mtoto, na hadi umauti unamfika, alikuwa akiishi kwenye nyumba yao ya familia