Monday , 19th Jun , 2023

Kura zinahesabiwa nchini Mali, kufuatia kura ya maoni juu ya katiba mpya ambayo inapanga mchakato wa kuirudisha nchi hiyo katika utawala wa kiraia wa kidemokrasia.

Viongozi wa kijeshi waliotwaa madaraka mwaka 2021 wamesema watakabidhi serikali iliyochaguliwa mwaka ujao.

Marekebisho hayo ya  katiba yanajumuisha bunge jipya la pili ili kuongeza uwakilishi nchini Mali.Wakosoaji wanasema hali hiyo  itamuacha rais akiwa na nguvu nyingi  na kwamba jeshi halipaswi kuwa na jukumu katika kuirekebisha katiba. Matokeo ya awali ya mchakato huo yatatolewa siku ya Jumanne.

Vituo vya kupigia kura vilifungwa mjini Bamako, Mali, saa 10:00 jioni siku ya Jumapili (Juni 18) ili kuanza kuhesabu kura. Katika siku hiyo, wananchi walipiga kura ya katiba mpya. Hatari ya mashambulizi ya kijihadi ilikuwa ni suala linalozingatiwa katika maeneo ya kati na kaskazini, ikimaanisha kuwa kura hiyo haikufanyika katika baadhi ya maeneo ya nchi, ikiwa ni pamoja na mji wa Kidal, ngome ya waasi wa zamani.

Timu ya waangalizi kutoka makundi ya asasi za kiraia yanayoungwa mkono na Umoja wa Ulaya imeripoti kuwa kulikuwa na masuala machache tu ya upigaji kura katika vituo vya kupigia kura ambavyo vilipelekwa.