
Akizungumza katika mkutano wa wananchi kwa dhamira ya kusikiliza kero na kutatua changamoto kadhaa ambazo aliwaahidi wanamtama, Nape anasema kwasasa watu wengi wamekubali kupotoshwa na kudemka na siasa, jambo lililoruhusu chuki baina yao ilhali viongozi wakuu wa vyama vya siasa maisha yao yanaenda na wanapatana.
Katika mkutano huo, Nape amegawa mitungi na majiko 254 ya gesi kwa wanawake wa umoja wa UWT ikiwa ni ahadi yake ya kuwakwamua na adha ya matumizi ya mkaa na kuni, huku akiiweka bayana dhamira yake ya kugawa mitungi hiyo kwa idadi kubwa ya wanawake Kwenye halmashauri yam tama bila kuangalia itikadi za vyama.
Nao wananchi, wamempongeza waziri nape kwakuwa mstari wa mbele kuhakikisha afya zao zinakuwa salama kwani wamekiri kupata shida kubwa kwenye matumizi ya mkaa na gesi ki afya, lakini pia wamesema ni sehemu moja wapo ya kuhakikisha wao wanatunza manzingira.