Tuesday , 13th Jun , 2023

Uongozi wa kituo cha mabasi cha Makumbusho kwa kushirikiana na madereva wa mabasi ya daladala na makondakta wamepiga marufuku vijana wanaopiga debe ndani ya kituo hicho ikiwa ni jitihada za  kudhibiti wizi kwa abiria wanaotumia kituo hicho

Wakizungumza na EATV madereva wa mabasi ya daladala na Makondakta wamesema mara baada ya marufuku hiyo vijana hao sasa wamekimbilia kwenye vituo vidogo vidogo  vya mabasi ya daladala hasa vile vilivyopo barabarani ingawa wameeleza wanapojaribu kutaka kuingia ndani ya mabasi hayo wamekuwa wakiwazuia

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati za ulinzi na usalama katika kituo hicho amesema hatua hiyo imekuja baada ya hapo nyuma kuwepo kwa matukio ya wizi hivyo kwa sasa suala Hilo limedhibitiwa

Hata hivyo meneja msimamizi wa kituo hicho Haidary Salum amesema mpango wa serikali na kituo hicho ni kuhakikisha hakuna wizi unaotokea ndani ya kituo hicho ikiwemo abiria kutibiwa