Tuesday , 6th Jun , 2023

Umoja wa Vijana wa CCM wilaya ya Ulanga unatarajia kufanya tamasha la kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa anazozifanya katika kuinua vijana kiuchumi kupitia ajira na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Viongozi wa UVCCM Ulanga

Mwenyekiti wa UVCCM wilayani humo Shahista Suleman, amesema tamasha hilo lina lengo la kumtia moyo Rais kutokana na kazi kubwa inayofanywa na serikali yake kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo hasa katika sekta ya afya, maji, elimu na ajira kwa vijana.

Naye Katibu wa Hamasa na Chipukizi wilaya hiyo Thomas Machupa amebainisha kuwa pamoja na mambo mengine wanaishukuru serikali na mbunge wa jimbo hilo kwa kuwawezesha vijana katika vikundi 7.