Thursday , 18th May , 2023

Jeshi la Polisi Mkoani Manyara, linawashikilia Mohamed Said na Diana Lozi wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa tuhuma za kukutwa na fedha halali za kitanzania zinazohisiwa kuwa ni za wizi na simu za mkononi 27 kwenye nyumba ya kulala wageni mjini babati

Kamanda wa Jeshi a Polisi mkoa wa Manyara, RPC George Katabazi ametoa wito kwa wananchi kutambua mali hizo akisema lengo ni kuvunja mtandao wa wizi ambao umekuwa ukiwaathiri wananchi katika maeneo mbalimbali hapa nchini

Katika hatua nyingine kamanda katabazi amewakamata watu wengine tofauti wilayani Kiteto kwa tuhuma za kukutwa na mitambo ya kutengeneza pombe haramu ya moshi (gongo) madawa y kulevya aina ya bangi na mirungi na fedha bandia kiasi cha sh laki 9