Tuesday , 16th May , 2023

Wafanyabiashara katika soko la Kariakoo wameendeleza mgomo wa kutofungua maduka kwa siku ya pili leo 

Hatua hii inakuja ikiwa imepita siku moja tangu Waziri Mkuu wa Tanzania atembelee soko hilo na kuahidi kukutana na wafanya biashara hao siku ya Jumatano kusikiliza kero zao

Wafanyabiashara hao wametangaza kuanza mgomo jana wakishinikiza baadhi ya mambo ambayo wanahisi hawatendewi haki na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ikiwemo matumizi ya nguvu katika ukusanyaji wa kodi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana ametangaza kusitisha kikosi kazi kilichoundwa kukusanya kodi katika soko hilo hadi utaratibu mwingine utakapotangazwa tena

Hata hivyo baadhi ya maduka leo yamefungwa pamoja na kwamba wafanya biashara hao waliahidi kufungua maduka yao kupisha mazungumzo yao na serikali siku ya jumatano

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Kariakoo Martin Mbwana ameviomba vyombo vya usalama kutoa ulinzi kwa wale ambao wapo tayari kufungua maduka yao kwa kuwa wamekuwa wakifanyiwa vurugu