
Kauli hiyo imetolewa ndani ya mkutano unaokutanisha mamalaka ya usafiri Aridhi LATRA na wadau wa usafirishaji kutoka kanda ya kaskazini ukilenga kutoa maoni ya rasimu ya kanuni mpya mamlaka hiyo
Suala kubwa linaloibuka ni wadau hao wa usafirishaji kushindwa kukubalina na baadhi ya kanuni hasa zile zinazogusa faini za barabarani na kuomba zipitiwe upya na kurekebishwa kabla ya kupitishwa
Kaimu mkurugenzi huduma za uchukuzi kitengo cha usafiri barabarani kutoka wizara ya uchukuzi Andrew Magombana ,anabainsha kuwa kanuni hizo zimewekwa ili ziweze kudhibiti usafirishaji na kuwa na utawala bora Pamoja na kulinda haki za watumiaji.
SB:Andrew Magombana-Kaimu mkurugenzi huduma za uchukuzi kitengo cha usafiri barabarani kutoka wizara ya uchukuzi.
Nae Mkurugenzi udhibiti wa barabara LATRA Johansen Kahatano anaeleza kuwa maoni yanayotakiwa kutolewa ni yale yanayolenga sekta ya usafirishaji pekee na kwamba yatafanyiwa kazi ambapo msisitizo unawekwa kwa wadau kusoma kanuni hizo vizuri ili waweze kuelewa
Kanuni hizo nane mpya za LATRA zimetungwa chini ya wizara ya uchukuzi sita zikiwa ni mpya ,ambapo zinahusisha masuala ya vizibiti mwendo, tiketi mtandao faini Pamoja na kanuni za vyombo vya kubebea bidhaa hatarishi