Thursday , 11th May , 2023

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita, limewaonya baadhi ya wananchi mkoani humo wanaoipiga namba ya dharura ya 114 kwa ajili ya kuwasalimia askari kama mchezo na kuwataka kuitumia namba hiyo pale wanapokuwa wanahitaji msaada wa uokozi pamoja na majanga mengine.

Kamanda wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji mkoani Geita Hamisi Dawa

Kamanda wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji mkoani humo Hamisi Dawa, amewataka wananchi hao kama wanataka kuwasalimia askari basi wafike kituoni hapo ili pia waweze kupata elimu sahihi ya matumizi ya namba hiyo.

"Namba hiyo ya 114 ina changamoto wengi wanaitumia vibaya unaweza ukawa umeshika laini kwa mtu mwingine unasalimia au kutoa maneno mwingine ana shida na hiyo simu, wasitumie kwa michezo hiyo simu, tutawachukulia hatua kali na ikiwezekana tutawafikisha mahakamani, wapige pale wanapokuwa na shida," amesema Kamanda Dawa