
Lukula amesema wanakumbuka JKT waliwafunga katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi lakini tumejiandaa kikamilifu kuhakikisha tunalipa kisasi.
Lukula ameongeza kuwa lengo lao ni kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu hivyo wanapaswa kukusanya alama tatu katika kila mchezo.
“Ni mchezo mgumu, walitufunga mchezo wa kwanza tunataka kwenda kulipa kisasi ingawa tunafahamu tutapata upinzani mkubwa.”
“Tumejipanga vizuri kuhakikisha tunakusanya pointi zaidi ili tuzidi kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wetu,” amesema Lukula.
Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu utapigwa kesho saa 10 jioni katika Uwanja wa Meja Genarali Isamuhyo uliopo Mbweni.