
Baadhi ya wawekezaji hao wamesema zipo mbinu mbalimbali katika kupanga kukuza mitaji kukuza uwekezaji katika mitaji ikiwemo kuweka fedha bila kutoa kwa kipindi fulani miezi 6 ama 12 ili kutengeneza riba fulani ambayo itahesabika kama faida uanzishwaji wa kampeni mbali mbali za mara kwa mara ambazo zitalenga kutangaza uwekaji akiba na ukopaji ulio rahisi
Katika mazungumzo na wataalaam hao wa fedha kutoka Taasisi ya fedha ya Mwanga Hakika wamesema kila taasisi za kifedha zimekuwa na fursa mbali mbali na nyingi zikiwa zimeshusha riba zao kwa ajili ya kuvutia wateja sambamba na kuwasaidia wananchi
"Uanzishwa wa kampeni z mara kwa utasaidia taasisi za kifedha kukua lakini pia kuboresha maisha ya wateja wao hivyo niwasisitize tu wananchi kuwa na tabia ya kutembelea taasisi hizo kujua kampeni walizonazo na huduma ambazo wao wanaweza kunufaika nazo"Amesema Projest Massawe Mkuu wa idara ya biashara Mwanga Hakika
Imeelezwa kuwa wajasiriamali walio wengi hushindwa kufafanua juu ya maneno vigezo na masharti kuzingatia na kujikuta wengi wakitumbukia katika mikopo isiyo na manufaa kwao na kuishia kushindwa kukua kibiashara.