
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde katika jukwaa la kilimo kwa ukanda wa Afrika mashariki na kusini mwa Afrika ambapo Tanzania ni mwenyeji wa mkutano huo ulioanza leo jijini Dar es salaam huku serikali ikipanga kununua ndege ya kumwagilia dawa mashambani
Mavunde amesema takribani mabonde 22 yote utekelezaji umeanza nchi nzima ikiwa ni jitihada za kupambana na ukame pamoja na mabadiliko ya Tabia nchi
Kwa upande wake Mwenyekiti wa SACAU ambao hujumuisha ukanda wa nchi za SADEC Dkt Yusuph Sinare amesema mkutano huo umewakutanisha wafadhili kwenye sekta ya kilimo IFAD ili kurekebisha sekta ya Kilimo hususani kwa vijana ambao ndio walengwa wa serikali kwa masilahi mapana yao na Taifa
Uanzishwaji huo wa mabwawa unatarajiwa kutunza lita bilioni 111