
Picha ya Rayvanny na Zuchu
Katika kipengele cha msanii bora wa kiume Africa Mashariki Rayvanny amewapiga chini wasanii Diamond Platnumz, John Frog - South Sudan, Khaligraph Jones - Kenya, Eddy Kenzo - Uganda, Otile Brown – Kenya, Meddy – Rwanda na Sat B - Burundi.
Kwa upande wa msanii bora wa kike Africa Mashariki Zuchu amewashinda Maua Sama, Nandy, Femi One, Sanaipei Tande na Jovial kutoka Kenya, Sheebah Karungi na Winnie Nwagi wa Uganda.