
Kufuatia takwimu hizo wadau wa usafirishaji,wafanyabiashara kutoka nchi za jumuiya ya Afrika mashariki kupitia baraza la wafanyabiashara EABC wamekutana kujadili namna bora ya kutumia bandari zilizopo kwenye nchi wanachama,kuja na majibu ya pamoja kuhusu sera za kibiashara kati ya nchi na nchi ili kuondoa vikwazo ambavyo vinasababishwa na watendaji katika mipaka,bandari na vituo vya forodha.
Wakibainisha hali ilivyo kwa sasa wamesema bado shida ni kubwa kwenye ufanyaji wa biashara kwa nchi za Afrika mashariki licha ya wakuu wa nchi hizo kukutana mara kwa mara.
Wamesema nchi wananchama wanafanya kazi ya kuzalisha bidhaa,mazao lakini bila kubadilisha utaratibu wa namna ya kusafirisha bidhaaa hizo nyingi zimekuwa zikikwama mipakani kutokana tuu na watu kufanya majuku yasiyo yao ama kwa maksudi kabisa.
Mkutano huo wa siku mbili umekutanisha wadau wa bandari,sekta binafsi,wafanyabiashara wasimamizi kutoka serikali za nchi wanachama kujadili jumuiya zingine zimefanuikiwaje kukuza chumi na biashara zao.