
Kiwango hicho cha fedha, kinajumuisha fedha zilizopangwa kutoka Bajeti ya mapato kwa mwaka huo, kiasi cha Billion 1,115,607,800.00 pamoja na fedha za marejesho ambazo nazo zimeingia katika mzunguko wa ukopeshaji.
Akikabidhi mfano wa hundi zenye thamani ya shillingi million 377 kwa vikundi 43 (Wanawake vikundi 31 wakipokea jumla ya shillingi million 266, Vijana vikundi 6 Tsh. 83 M na wenye ulemavu vikundi 6 Tsh. 28 M), ambapo vinahitimisha awamu ya nne ya utoaji kwa mwaka 2021/2022.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdulrahman Shiloow amewataka wanavikundi hao kuzingatia mipango yao na kufanya biashara zenye tija ili warudishe mkopo na kupata faida ya kazi na kubadili hali zao za maisha.
Amesema fedha hizo sio za bure, ni mkopo, hivyo wanapaswa kufanya utafiti wa biashara sio kuiga kwa mwingine.