Friday , 28th Oct , 2022

Kampuni ya michezo ya kubahatisha Parimatch imefanya maboresho makubwa katika tovuti yao ya kubashiri, ambayo kwa sasa itawawezesha wateja wao kusuka mikeka yao na ku-share kwa marafiki zao huku wakiwa wanatumia intaneti kidogo wakati wa kuperuzi na kasi kubwa.

Hayo yamebainishwa na Afisa Habari wa Parimatch Tanzania, Ismael Mohamed wakati alipokuwa akizundua rasmi jukwaa hilo la kubashiri mtandaoni kupitia PARIMATCH na kusema kwamba imekuwa ni desturi yao kusikiliza maoni ya wateja wao kila mara na kuamua kuyafanyia uamuzi ili kusudi waweze kuwapatia kitu kilichokuwa bora wateja wao ambao hutumia muda wao ziada kujiburudisha akili zao na Parimatch.

 

“Tumefanya mabadiliko mazuri, tumerekebisha mambo mengi. Katika kipindi hiki ambacho tunaelekea katika michuano mikubwa ya Kombe la Dunia sisi kama Parimatch, tumeona wateja wetu wanastahili kupata kitu kizuri chenye speed ya uhakika ili wanapokuwa wanapata burudani basi na beti zao ziendane na kasi ya mchezo”, amesema Ismael.

 

“Licha ya kwamba tumebadilisha tovuti yetu kwa sasa lakini wateja wetu wote watatumia taarifa zao za zamani kuingia www.parimatch.co.tz na wataiona Platform yetu mpya yenye muonekano wa kijanja na wenye kuvutia kwa hakika”

 

Aidha, Ismael amesema katika maboresho hayo ambayo Parimatch imefanya katika kipindi hiki, yataweza kuwaruhusu watumiaji wa simu za android kuitumia kwa njia ya application kwa urahisi na ufanisi mkubwa zaidi.

Pamoja na hayo, Ismael pia aliwasisitizia wadau wa Parimatch kuendelea kufurahia kucheza Virtual game na michezo mingine mbalimbali kupitia tovuti yao ambayo itaweza kukuburudisha na kusisimua.