Wednesday , 26th Oct , 2022

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maendeleo na kasi ya ujenzi wa mabehewa mapya kwa ajili Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli Tanzania yanayotengenezwa na kampuni ya Sung Shin Rolling Stock (SSRT) iliyoko nchini Korea Kusini

Majaliwa ameyasema hayo mara baada ya kutembelea kampuni ya SSRST inayotengeneza mabehewa na injini za treni nchini Korea Kusini.

Aidha, Majaliwa ametembelea kituo cha Seamul Undong  ambacho ni taswira ya maendeleo ya Korea kupitia mpango wa kuviwezesha vijiji ambao unatekeleza mpango huo nchini Tanzania katika mkoa wa Morogoro (Pangawe) na Zanzibar ambapo amemshukuru Rais wa Kituo hicho na kumuomba kuendelea kutoa ushirikiano.