Monday , 17th Oct , 2022

Shirika la mpango wa maendeleo la umoja wa mataifa UNDP limesema Tanzania ina vijana wengi wenye mawazo mazuri ya kibunifu lakini wanashindwa kuyaendeleza kwasababu hawana mbinu za kurasimisha ubunifu wao.

Wadau wa ubunifu wakiwa na mkurugenzi wa Sahara Ventures

Ujumbe wa shirika hilo umetolewa na Meneja mkazi wa  mpango wa miradi ya kuwaezesha vijana wabunifu,  kufikia malengo yao ya kurasimisha mawazo bunifu kuwa biashara ambapo amesema shirika hilo kupitia mradi wake wa funguo Innovation linakusudia kuwasaidia wabunifu wengi zaidi kibiasharisha na mawazo yao.

Tayari kongamano la vijana wabunifu limetambushwa likiwa na lengo la kuwakutaniaha vijana wabunifu, wataalam  pamoja na wawekezaji, huku dhumuni likiwa ni  kujadili kwa kina, na kuweka mikakati ya pamoja ya jinsi gani teknolojia, ubunifu na ujasiliamali unaweza kuwasaidia vinana wabunifu kufikia malengo yao.

Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku nne kuanzia Jumanne hii Oktoba 17, 2022 na litashirikisha vijana zaidi ya elfu tatu wa ndani na nje ya ambapo pamoja na mambo mengine vijana wenye mawazo bunifu watafundishwa mambo kadhaa ikowe mbinu za kurasimisha ubunifu wao kuwa biashara halisi.