Wednesday , 12th Oct , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi wa Kongamano la Nishati safi ya Kupikia yaani 'Clean Cooking Conference' ili kuchunguza vikwazo vinayodumaza matumizi y

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Kongamano hilo linalenga kupendekeza mikakati ya kufanikisha upatikanaji wa nishati safi, za bei nafuu na endelevu nchini Tanzania.

Mkutano huo utafanyika tarehe 1 na 2 Novemba 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha watunga sera, wadau wa maendeleo, wajasiriamali, wawekezaji, wafadhili, wanataaluma na wananchi kwa ujumla.

Waziri Makamba aliongeza kwa kusema asilimia 63.5 ya kaya zote nchini hutumia kuni kupikia na asilimia 26.2 hutumia mkaa sehemu iliyobaki inajumuisha asilimia 5.1 ya kaya zinazotumia gesi za mitungi, asilimia 3 umeme, na asilima 2.2 ikiwa ni nishati nyingine.

''Kupika ni moja ya tukio pekee linalounganisha watu wa hali zote: wa juu, kati na chini, ila Watanzania wengi hatujui na wala hatuhoji aina ya nishati inayotumika katika kupika vyakula tunavyokula kila siku'' - Amesema Waziri Makamba.