
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro
Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba 3, 2022, wakati akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha Makamanda wa Polisi wa takribani mikoa minne, kuzungumzia hali ya usalama katika mikoa yao na namna ya kudhibiti vikundi vya uhalifu.
"Haya makundi kwa nyakati tofauti tofauti yalikuwa na majina tofauti, kuna kipindi hawa panya road walikuwa wanaitwa komando yoso, baadaye wakawa wanaitwa kiboko msheli, kuna kipindi makundi na watu wenye hulka hii hii walikuwa wanaitwa kumi ndani, kumi nje," amesema Kamanda Muliro
Tazama video hapa chini kwa undani zaidi