Tuesday , 27th Jan , 2015

Wafanyakazi wa hosipitali ya wilaya  ya Monduli mkoani Arusha  wamejitolea  kuwanunulia  wagonjwa mashuka  100 ili kupunguza makali ya tatizo hilo  linaloikabili hosipitali hiyo.

Muonekano katika wodi ya wagonjwa hospitali ya wilaya ya Monduli mkoani Arusha

Wakizungumza  wakati wanakabidhi mashuka  hayo  kwa uongozi wa hosipital  watendaji  hao wamesema kuwa wamefikia hatua  hiyo  baada ya kuona ahadi ya serikali ya kutatua tatizo hilo inachelewa na wagonjwa wanaendelea kuteseka.

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali hiyo  Dkt Engai Edward amewashukuru watendaji hao  na kuwataka wadau wengine pia kuona umuhimu wa kusaidia  matatizo mengine  badala  ya kusubiri serikali.

Nao baadhi ya wananchi wamepongeza hatua ya wafanyakazi  hao ya  kukerwa na shida  zinazowakabili wananchi hasa wagonjwa na kujitolea kuwasaidia  na wamewaomba watendaji wa idara zingine kuiga mfano huo.