Sunday , 4th Sep , 2022

Serikali imekanusha uzushi uliotolewa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema na sekta ya elimu kwa kusema shule nchini zitafunguliwa Septemba 21 jambo ambalo si sahihi na wala hakuna muongozo wala maelekezo hayo.

Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda

Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda, amesema ratiba ya kufunguliwa kwa shule nchini iko vilevile ambapo shule zitafunguliwa kesho Septemba 5, 2022.

"Naomba mpuuze jambo hili kwanza aliyesambaza anatumia nembo ya kampuni moja ambayo kampuni hiyo haijui na haihusiki na tangazo hilo, kwahiyo hakuna maelekezo yoyote zaidi ya yale yaliyotolewa na Kamishna wa Elimu” Amekaririwa Waziri Mkenda

Kuhusu mageuzi ya elimu, Waziri Mkenda amesema kuwa serikali inafanya mapitio ya sera ya elimu ya mwaka 2014 pamoja na mapitio ya mitaala ili kuboresha sekta ya elimu.