Saturday , 3rd Sep , 2022

Mwili wa Amina Hassan (34) aliefariki kwa kuchomwa visu sehemu mbalimbali za mwili na mume wake Mashaka Jeremia umeagwa leo kwenye makazi yake mtaa wa Lukilini kata ya Kalangalala mkoani Geita na kusafirishwa mkoani Dodoma kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika wilayani Chamwino.

Amina alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Geita baada ya kuchomwa visu zaidi ya mara 10 na mme wake usiku wa Agosti 30, 2022, na ameacha watoto wawili wa kike.

Baadhi ya majirani wamesema wanandoa hao walikuwa na mgogoro juu ya kukutana kimwili ambapo walishauriwa na daktari wasikutane kwa muda kutokana na changamoto za kiafya zinazowakabili, hivyo mwanaume alikataa ushauri wa daktari na amekuwa akitumia nguvu kumuingilia mkewe.

Majirani wanasema wawili hao walikuwa wametengana vyumba vya kulala kutokana na mwanaume alikataa ushauri wa kutumia dawa walizoashauriwa na madaktari