Thursday , 1st Sep , 2022

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema kwamba ni lazima kila mtu mwenye kipato alipe kodi ili kutotengeneza mwanya mkubwa kati ya wasio nacho na wenye nacho hapa nchini.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba

Kauli hiyo imetolewa hii leo Septemba Mosi, 2022, jijini Dodoma, na waziri wa Fedha na Mipango Daktari Mwigulu Nchemba, wakati akitolea ufafanuzi kufuatia malalamiko ya wananchi juu ya tozo mbalimbali wanazotozwa hususani kupitia miamala ya benki.

"Ni lazima mtu ambaye ana mapato anatakiwa alipe kodi tena iliyo sahihi, aliye na kidogo alipe kidogo aliye na kikubwa alipe kikubwa hiyo ndiyo ambayo utatoza kwa tajiri usomeshe mtoto wa maskini, ukitaka maskini abebe mzigo utatengeneza pengo la walio nacho na wasio nacho kuwa kubwa na kwenye nchi si jambo jema," amesema Dkt. Nchemba