Wednesday , 20th Jul , 2022

Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kamishna wa Polisi Camilius Mongoso Wambura kuwa Inspekta na Mkuu wa Jeshi la Polisi akichukua nafasi ya Simon Sirro ambaye ameteuliwa kuwa balozi nchini Zimbabwe

Wambura alikuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) 

Aidha Rais Samia amemteua aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Simon Sirro kuwa balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe

Katika hatua nyingine Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhan Hamisi Kingai na kumteua kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Kingai anachukua nafasi ya Camilius Wambura ambaye ameteuliwa kuwa IGP