
Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi Ramadhani Kingai amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa katika kijiji cha kabulanzwili kata ya Kurugongo ikiwa ni sehemu ya operesheni ya jeshi hilo kudhibiti matumizi biashara ya madawa hayo.
Katika hatua nyingine jeshi hilo kupitia opeshesheni zake katika kipindi cha kuanzia tarehe kumi mwezi huui limefanikiwa kukamata watuhumiwa watuhumiwa themanini na tano yakiwemo ya mauaji, Ubakaji, na uhamiaji haramu.
Kamanda Ramadhani Kingai amewataka wakazi wa mkoa wa Kigoma kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pindi wanapohisi ama kubaini uwepo wa watu wanajihusisha na uhalifu.