Tuesday , 12th Jul , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba juzi Waziri Mkuu alimwambia kuna maradhi yamejitokeza katika mikoa ya Kusini ya watu kuvuja damu puani na kudondoka, ambapo sasa wataalam wapo huko ili kuchunguza kujua ni kitu gani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia ametoa kauli hiyo hii leo Julai 12, 2022, jijini Dar es Salaam, wakati wa madhimisho ya miaka 20 ya AMECEA.

"Nilikuwa nazungumza na Waziri Mkuu juzi ametoka ziara Lindi ananiambia ameona kuna maradhi yameingia wanadamu wanatokwa tu damu za pua na wanadondoka, hatujui ni kitu gani, wanasayansi na wataalamu wa afya wamehamia huko wanaangalia ni kitu gani," amesema Rais Samia

Aidha Rais Samia ameongeza, "Kwanini mwanadamu atokwe tu na damu za pua adondoke, angekuwa mmoja wawili tungesema presha imepanda vein zimeburst, lakini ni wengi kwa mfululizo ni maradhi ambayo hatujawahi kuyaona na yote kwa sababu tunaharibu makazi ya viumbe kule waliokoumbwa na Mungu tunawasogeza kwetu wanatuletea hiyo aina ya maradhi,".