
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu George Simbachawene, wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Mbuga jimbo la Kibakwe Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
"Hata kama watu watatoka ni vizuri akabaki mtu mwenye kumbukumbuku za watu waliolala katika nyumba yake ili kupata takwimu sahihi," amesema waziri Simbachawene
Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene, ameeleza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan, na kutoa kiasi cha shilingi million 100 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo elimu na barabara.