
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Omari Kipanga amewataka walimu waliopatiwa mafunzo na chama cha Scouts Tanzania kwenda kuyatumia mafunzo waliyoyapata kufundishia nyimbo za kizalendo ikiwemo wimbo wa Taifa na wa Afrika mashariki
Pia Naibu waziri Kipanga amewaagiza walimu waliopatiwa mafunzo ya Scouts Nchini kwenda kuanzisha vikundi vingi vya chama hicho kwa lengo la kuendelea kudumisha uzalendo uwajibikaji pamoja na kuendelea kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya ambayo yamekuwa yakipoteza nguvu kazi ya Taifa.
Naibu waziri Kipanga ametoa maagizo hayo wakayi akifungua semina ya siku tano inayotolewa na chama cha scout Tanzania kwa walimu wa shule za msingi inayofanyika Mkoani Tanga.
"Kuteuliwa kuja kupata mafunzo haya mkiwakilisha halmashauri zenu nendeni mkafundiahe katika kukuza uzalendo na tutafwatilia kwa karibu kufanya tathmini kuona mna enda kuyafanyia kazi nawaagiza kila Mwalimu aliyepata mafunzo haya akaanzishe vikundi vya Scouti mashuleni ili kuwafanya vijana wetu kuwa wazalendo kuheshimu nyimbo zatu ikiwa wimbo wa Taifa na Afrika mashariki"
"Vijana wetu wamekuwa wahanga wakubwa wa madawa ya kulevya naomba mjue kuwa vijana wetu wanaharibika na badala yake kuwapongeza kabisa tumieni mafunzo hayo kueleza athari zake kwahiyo tuna Kazi kubwa ya kufanya " alisema Kipanga