Thursday , 7th Jul , 2022

Kamisaa wa Sensa Anna Makinda, amesema baadhi ya Watanzania wanapenda uongo kutokana na maneno ya uzushi yanayozagaa mitandaoni kwamba majina ya wasimamizi wa sensa hayatoki kwa sababu wameweka watoto wao, na kusema majina yakitoka waombaji wote wenye sifa watachukuliwa.

Kamisaa wa Sensa, Anna Makinda

Kauli hiyo ameitoa hii leo Julai 7, 2022, mkoani Katavi, wakati akizungumzia suala hilo la kutangazwa kwa majina ya wasimamizi wa sensa.

"Tanzania tunapenda sana uongo, eti wameweka watoto wao nani kawaambia tumeweka watoto wetu, bado majina hayajatoka sababu tunafanya kazi kwa umakini," amesema Kamisaa Makinda

Aidha Mama Makinda, amewatoa hofu waombaji kuwa wote wenye sifa watachukuliwa kutokana na uhitaji uliotangazwa na serikali, "Watu laki mbili na elfu tano ndio wanaotakiwa kwa ajili ya kazi ya Sensa ila mpaka sasa tumepokea maombi zaidi ya laki sita,".