Friday , 17th Jun , 2022

Katika kuunga mkono kampeni ya Namthamini na kuhakikisha mtoto wa kike hakosi masomo kwa kukosa taulo za kike, wadau wetu chuo cha Kilimanjaro Institute of Technology and Management (KITM) leo walituletea mchango wa taulo za kike pakiti 128.

kutoka kushoto Mkutubi wa chuo cha KITM, Dorotea Tobias na Mkuu wa chuo hicho Ahmed Mbezi wakikabidhi taulo za kike kwa mtangazaji wa East Africa TV, Mwanne Othman.

Ahmed Mbezi ambaye ni Mkuu wa chuo hicho amesema wametoa mchango huo ili kutimiza ahadi yao waliyoitoa kupitia kipindi cha DADAZ kwamba watahakikisha wanachangia katika kampeni ya Namthamini ili kuweza kuwasaidia watoto wa kike kubaki shuleni kipindi wakiwa kwenye siku zao za hedhi.

 

Mchango wa pakiti 128 za taulo za kike walizotoa zitaweza kuwasaidia wanafunzi 13 kwa mwaka mzima.

Kwa upande wake Dorotea Tobias ambaye ni Mkutubi amesema watoto wa kike wana thamani kubwa katika nchi na ni wakina Samia wengine, ndiyo maana wao kama chuo wameguswa na kampeni hii na kuchangia.