Akikabidhi fedha hizo kwa niaba ya Rais Samia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amemsisitiza Kijana Yassin kutumia fedha alizopatiwa kujiimarisha kiuchumi ili lengo la Rais kutoa fedha hizo liweze kutimia.
Kwa upande wake Yassin Said amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa msaada aliopatiwa na kuahidi kuzitumia kwa lengo lililokusudiwa.



