Tuesday , 7th Jun , 2022

Mbunge wa jimbo la Mbogwe, Nicodemus Maganga, amemuomba Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, kama kuna mahali popote basi afungulie ili wananchi waweze kupata pesa na zijae kwenye mifuko yao kwani wana hali ngumu.

Mbunge wa jimbo la Mbogwe, Nicodemus Maganga

Kauli hiyo ameitoa hii leo Juni 7, 2022, wakati akichangia hoja ya makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango iliyowasilishwa hii leo na waziri wake.

"Kweli tunasema hali sasa hivi ina kaunafuu lakini bado hali ni ngumu, sasa kwa vile wewe ni Waziri wa Fedha (Mwigulu Nchemba) angalia kama kuna sehemu yoyote fungulia fedha ili kusudi hata kwa wanyonge zijae mifukoni maana kwenye kampeni huwa tunasema tunawapigani wanyonge, sasa wanyonge bado hawajapata hela," amesema Mbunge Maganga.

Tazama video hapa chini