Vyombo vya habari huko Florida vinamtafuta abiria huyo kwa ushujaa wake
Ndege hiyo ndogo ya injini moja ilikuwa na rubani mmoja na abiria wawili. Baada ya rubani kupoteza fahamu abiria mmoja alienda katika sehemu ya rubani na kupiga simu kuomba msaada.
Simu yake ilipokelewa na waongoza ndege wa uwanja wa ndege wa Palm Beach katika mji wa Florida na kumpa maelekezo mpaka akafanikiwa kufika katika uwanja huo na kutua salama bila tatizo lolote kutokea.