Baraza la wazee wa klabu ya soka ya Yanga limesema kitendo cha Manispaa ya Ilala kutotoa jibu juu ya maombi ya timu hiyo kutaka eneo zaidi la kujenga kitega uchumi cha Yanga Jangwani city ambako pia kutajengwa uwanja wa kisasa wa timu hiyo ni kitendo cha uonevu
Katibu mkuu wa baraza hilo mzee Ibrahim Akilimali amesema uongozi wa Yanga ulishakamilisha taratibu zote kwa mamlaka husika za ardhi na kinachokwamisha ni jibu la mwisho kutoka Manispaa ya Ilala jibu ambalo waliahidiwa kupewa tangu mwaka jana
Kwaupande mwingine kufuatia hali hiyo mzee Akilimali akaenda mbali zaidi na kulitaka baraza la madiwani la manispaa ya Ilala chini ya mstahiki meya wake kuhakikisha wanatoa majibu haraka ya ombi hilo la yanga kwa ajili ya ujenzi huo
Akilimali ametuma ombi hilo kwa Meya wa Ilala akimtaka kutambua kuwa kitega uchumi hicho kitakua faida si kwa yanga pekee bali na kwa watanzania wote kwa ujumla
Na Baraza hilo pia limetoa siku tano ili kupata majibu hayo toka manispaa ya Ilala na vinginevyo watafanya maandamano yakupeleka malalamiko yao kwa mkuu wa mkoa ama kwa Rais.