
Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa
Waziri Bashungwa amechukua hatua hiyo kufuatia uamuzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, wa kupiga marufuku bodaboda na bajaji kuingia katikati ya Jiji hilo isipokuwa kwenye maeneo yaliyoainishwa.
"Bila shaka nia ni njema, ila dosari ipo kwenye handling jambo lenyewe, serikali yetu ya awamu ya sita inatambua na kuthamini ajira za vijana wetu za bodaboda na bajaji kuwa ni ajira rasmi na wanajipatia riziki na familia zao," amesema Bashungwa
Aidha Waziri Bashungwa akaongeza, "Namuelekeza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla, kusimamia usitishwaji wa zuio hilo ili kutoa nafasi ya kufanya tafakuri zaidi'|.