
kombe la Uefa champions league
Manchester City wamepoteza mchezo mmoja kati ya tisa waliocheza kwenye hatua ya makundi wakishinda 7 na sare 1 huku wakipoteza kwenye mchezo wa finali dhidi ya chelsea huku tangu msimu wa kwanza wa kocha Joseph Guardiola wa 2016/17 atue ndani ya City ana asilimia kubwa ya ushindi kuliko klabu nyingine yoyote wakiwa na wastani wa asilimia nje ya hatua ya makundi (64% - 14/22).
Mkufunzi Diego Simeone wa Atlético Madrid alimuondoa Joseph Pep Guardiola kipindi akiwa Bayern Munich kwenye hatua ya nusu fainali msimu wa 2015-16 ndani ya UEFA Champions League kwenye sare ya magoli (2-2 ) na kuvuka kwa goli la ugenini huku magoli 2 yakipatikana kwenye mashuti 18 yaliyopigwa na Atletico huku Bayern wakifunga magoli 2 kwenye mashuti 53 waliyopiga
Kevin De Bruyne anaongoza kwa kupiga pasi za mwisho yaani assist (kapiga mara 17) huku iwapo akicheza huu utakuwa ni mchezo wake wa 50 ndani ya UEFA Champions League tangu atue kwenye viunga vya Etihad mnamo msimu wa 2015-16 huku Antoine Griezmann kwenye michezo 55 ndani ya UEFA Champions League amefunga magoli 25 ilhali kwenye michezo sita ya nyuma amefunga magoli 4 na kutoa pasi za mwisho mara mbili
Nyota wa Real Madrid Vinícius Júnior amehusika kwenye mashuti 44 yaliuopigwa langoni kwa wapinzani akifatiwa na kiungo wa Manchester City’s Riyad Mahrez ambaye amehusika mara 42 huku mashuti yakiwa 29 na akitengeneza nafasi za magoli mara 13 huku mlinda mlango wa Atletico Jan Oblak kwenye michezo 67 hajaruhusu wavu wake kutikiswa kwenye michezo 30 tangu aanze kuitumikia klabu hiyo msimu wa 2014/15