Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani kuanzia saa kumi jioni ikiwemo wadau mbalimbali wa soka kutakiwa kujitokeza ili kuweza kushuhudia mchezo huo.
Ofisa Habari wa Coastal Union, Oscar Assenga amesema kuwa mechi hiyo ni sehemu ya kuhakikisha kikosi hicho kinajiimarisha zaidi kila idara kabla ya mchezo wake na Polisi Morogoro.
Assenga amesema kuwa maandalizi ya kuelekea mchezo huo yamekamilika kwa asilimia kubwa na Mombasa Combain wanatarajiwa kutua leo jijini hapa tayari kwa ajili ya mechi hiyo itayochezwa kesho kuanzia saa kumi jioni.
Hata hivyo aliwataka wapenzi wanachama na mashabiki wa soka kuhakikisha hawakosi fursa hii adimu kuja kuishuhudia timu yao ikicheza kwenye uwanja wake wa nyumbani kabla ya kuanza mechi za Ligi kuu zinazofuata.
Wakati huo huo,Kikosi cha timu ya Coastal Union kinaendelea na mazoezi kila siku kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly na sasa kipo tayari kuweza kuikabili timu yoyote ile itakayokutana nayo na kuweza kupata matokeo mazuri.