Tuesday , 29th Mar , 2022

Watu 6 wamefariki Dunia  katika ajali ya gari na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo  katika eneo la  Nyasa Barabara ya kutoka Lushoto kwenda Mombo.

Picha kutoka eneo la tukio

Ajali hiyo imehusisha Fuso  yenye namba za usajili T 239 AFD lililokuwa limebeba bidhaa za sokoni kutokea Wilaya ya Lushoto kwenda Handeni.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa kwa taarifa za awali watu 4 ndio waliopoteza maisha na baadaye waliongezeka wengine wawili ambao walikuwa majeruhi. 

"Waliotutoka mwanzoni walikuwa wanne lakini wameongezeka majeruhi wawili na jumla kufikia 6 ambapo kati yao waliofariki wanaume ni 4 na wanawake ni wawili," amesisitiza Kamanda Jongo.